Home ๐ŸŽฌ Bollywood ๐ŸŽต Pakistani ๐ŸŽค English Pop

Mtaniona Hivi Hivi

๐Ÿ‘ค Jahazi Modern Taarab โ€ข ๐ŸŽผ Mpenzi Chocolate โ€ข โฑ๏ธ 12:32
๐ŸŽต 2098 characters
โฑ๏ธ 12:32 duration
๐Ÿ†” ID: 13275926

๐Ÿ“œ Lyrics

Jua ulianza ufizi ndio meno yakaja
Namuamini mwenyezi ndie mtoa haja
Sitakonda ngozi kwa vitisho vya waja
Na wenu uchochezi na hizo bwabwaja
Kuharibu hamuwezi alopangiwa mja
Kazi ya mwenyezi ngumu kwa mja
Kama wangu kikazi nipo nawangoja
Kama ni wakwezi tungueni makoja

Aah heshima yangu imewatia kiburi mnanipaka matope
Na utu wangu umewatia ujeuri mnaona mnilipe
Aah heshima yangu imewatia kiburi mnanipaka matope
Na utu wangu umewatia ujeuri mnaona mnilipe

Aah basi wenzangu huo si ujabari hayo ni maruperupe
Aah maneno chungu na kuniwekea nadhiri mie ili niogope
Aah basi wenzangu huo si ujabari hayo ni maruperupe
Aah maneno chungu na kuniwekea nadhiri mie ili niogope

Nyie si mungu punguzeni mukari na yenu mapepe aah
Nikosa langu kukaa nanyi vizuri nikuarepe nikurepee
Nyie si mungu punguzeni mukari na yenu mapepe aah
Nikosa langu kukaa nanyi vizuri nikuarepe nikurepee

Mambo mengine nomaa washkaji hayapendezi
Majina kuchafuliana kwa sababu ya mapenzi
Mambo mengine nomaa washkaji hayapendezi
Majina kuchafuliana kwa sababu ya mapenzi

Japo ukweli Hanna aaaah mnamuudhi mwenyezi
Ohh mie mtaalamu sana aah ila kwa huyu siwezi
Japo ukweli Hanna aaaah mnamuudhi mwenyezi
Ohh mie mtaalamu sana aah ila kwa huyu siwezi

Kama mna hamu sana nnae wangu mpenzi
Wenyewe tunapendana anashona nadarizi
Kama mna hamu sana nnae wangu mpenzi
Wenyewe tunapendana anashona nadarizi

Mmenikuta muungwana
Nakuamini mwenyezi hivi hivi mtaniona kunishusha hamuwezi
Mmenikuta muungwana
Nakuamini mwenyezi hivi hivi mtaniona kunishusha hamuwezi

Mtaniona hivi hivi ooh mtaniona
Aah kwangu mtasubiri sana, mtasubiri sana

La kusema mimi sina na mayoni sina fundo kaniongoza subhna
Taratibu wangu mwendo hada ya mja hinena muungwana ni vitendo
Angali mungu anaona roho zenu zina fundo
Hivi hivi mtaniona sihofu vyenu vishindo
Sintojitia hashuo kusema yasio na maana msimamo Ndio huo
Mungu anatosha sana muungwana akivuliwa nguo hasimami huchutama
Oooh mtajibeba aaah mtajibeba
Siijali vishndo nyenu sihofu porojo zenu
Mmenipandisha mizuka tawile tawile tawilee
Aaah mzuka wangu umepandaaa tawile tawile tawilee

โญ Rate These Lyrics

โ˜†โ˜†โ˜†โ˜†โ˜†
Average: 0.0/5 โ€ข 0 ratings