Home ๐ŸŽฌ Bollywood ๐ŸŽต Pakistani ๐ŸŽค English Pop

Nchi Ya Kitu Kidogo

๐Ÿ‘ค Eric Wainaina โ€ข ๐ŸŽผ Sawa Sawa โ€ข โฑ๏ธ 4:38
๐ŸŽต 1160 characters
โฑ๏ธ 4:38 duration
๐Ÿ†” ID: 3187384

๐Ÿ“œ Lyrics

Mzee alisema hakuna cha bure
Huo msemo tunautafsiri kinyume ee
Hata shule kuingiza mtoto
Lazima utoe mchoto
Kupata simu ni balaa
Road license bei nafuu 'tanunua
Kupoteza ID ni mashaka, twarudisha jamhuri yetu nyuma
Nchi ya kitu kidogo, ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe ndugu, nenda Limuru(nenda Limuru)
Hata nyumbani ukipatwa na majambazi, kupigana naye wasema sisis hatuna gari
Lete elfu tano ya petroli, saidia utumishi
Mahakamani hela ndio haki
Kwa elfu chache mshtakiwa ndiye mshtaki,
Utajiri huwa ushahidi
Twarudisha jamhuri yetu nyuma

Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka soda ewe inspekta, burudika na Fanta
Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe mama, nunua ketepa
(Aha)
Huko Kenyatta madawa zimeisha
Masheet zauzwa marikiti mia kwa mia
Wafanyikazi waenda miezi bila pesa
Ni bahati ukitibiwa
Mzigo wetu unazidi kuwa mzito
Watoto wanne na mshahara wa elfu mbili
Mia tano ya vitabu viatu na vyakula, nauliza na Mbotela vje huu ni uungwana'
Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe ndugu nenda limuru
Nchi ya kitu kidogo
Ni nchi ya watu wadogo
Ukitaka chai ewe mama, nunua Ketepa(nunua Ketepa)

โญ Rate These Lyrics

โ˜†โ˜†โ˜†โ˜†โ˜†
Average: 0.0/5 โ€ข 0 ratings