Home ๐ŸŽฌ Bollywood ๐ŸŽต Pakistani ๐ŸŽค English Pop

Siri

๐Ÿ‘ค Walter Chilambo โ€ข ๐ŸŽผ Thank You Lord โ€ข โฑ๏ธ 3:56
๐ŸŽต 658 characters
โฑ๏ธ 3:56 duration
๐Ÿ†” ID: 3187797

๐Ÿ“œ Lyrics

Kama Mungu angechangua watu wake
Mimi singekuwepo duniani
Kama Mungu angechagua watakatifu
Mimi singekuwepo duniani

Mimi binadamu, wala si malaika
Mengi nimekosea na kukuchukiza
Mi nafanya mambo yasiyo stahili
Nimevuruga vuruga mipango yako
Wanihurumia

Mbele ya macho ya wanadamu
Nilikuwa nikijificha
Kumbe wewe waniona
Kwa kujifanya mtakatifu
Tena bingwa mkarimu
Tena mpole sana

Sikio lako, yanisikia
Siwezi jificha

Sasa nimetambua, mbivu na mbichi ni zipi
Sasa ninaelewa, njia salama ni wapi
Na nimejua bila ya wewe sifiki
Hata nikila pasipo neno lako sishibi

Neema yako, ila kwa neema yako
Upendo wako, kwa upendo wako
Rehema zako zimeniimarisha tena

โญ Rate These Lyrics

โ˜†โ˜†โ˜†โ˜†โ˜†
Average: 0.0/5 โ€ข 0 ratings